Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndugu Zainabu Tareck, akiwasili Shule ya Sekondari Kishapu kama moja ya vituo alivyopanga kutembelea katika ziara yake wilayani Kishapu katika shule zote za wilaya hio. Ziara hio imepokelewa vizuri na walimu wa shule yetu na kuchukuliwa kama ya Kipekee katika kuboresha elimu katika wilaya yetu. Karibu sana mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ndugu
Zainabu Tareck.
| Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndugu Zainabu Tareck akiwasili katika Shule ya Sekondari ya Kishapu. |
| Mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainabu Tareck akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari kishapu waliokuwa wakimkaribisha kwa heshima na taadhima. |
| Ndugu Zainabu Tareck akiteta jambo na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kishapu na Mkuu wa wilaya pamoja na Mkuu wa Shule ya Kishapu baada ya kuwasili shuleni hapo. |
| Ndugu Zainabu Tareck,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Kishapu kuhusu mustakabali wa masomo na maisha yao ya baadae. |
| Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Zainabu Tareck akitoa maagizo kwa Mkuu wa Shule, Ndugu Hosea Somi baada ya kumaliza ziara yake shuleni hapo |
| Baada ya kumaliza Ziara ya mkuu wa Mkoa Shuleni hapo, Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kishapu akielekea katika gari yake tayari kwa kuondoka. |